Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

ELIMU YA UKATILI WA WAZAZI DHIDI YA WATOTO YATOLEWA

Posted on: July 23rd, 2025

Kitengo cha Ustawi wa Jamii kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara  kimeendelea kutoa elimu kwa wananchi kupitia huduma ya Kigoda cha Mteja kwa lengo la kuongeza uelewa kuhusu masuala ya kijamii, hususa ni ukatili wa wazazi dhidi ya watoto.


Zoezi hilo la Elimu limefanyika leo Julai 23, 2025 Ambapo wananchi mbalimbali waliokuwa wamefika kuwatembelea ndugu au jamaa waliolazwa walipata fursa ya kushiriki katika mafunzo hayo ya wazi.Maafisa ustawi wa jamii walitoa elimu kuhusu namna ya kutambua dalili za ukatili unaofanywa na Wazazi Dhidi ya watoto ,athari zake kijamii na kisaikolojia, pamoja na hatua stahiki zinazopaswa kuchukuliwa kwa mujibu wa sheria na miongozo ya ustawi wa familia.