Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

DKT KATHERINE MAGALI AMETOA WITO KWA WANANCHI WA MKOA WA MANYARA KUFANYA VIPIMO VYA KIBINGWA

Posted on: May 1st, 2023
Leo ni Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo watumishi wa hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara wameungana na watumishi wa taasisi nyingine kuadhimisha siku hii iliyofanyika kimkoa Wilaya ya Babati na kuhudhuriwa na Viongozi wa Mkoa, akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Charles Makongoro Nyerere ambaye alikuwa ni Mgeni Rasmi.

Akizungumza Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Dkt. Katherine Magali baada ya kupewa nafasi, ametumia fursa hii kuwakumbusha wananchi wa Mkoa wa Manyara kuja kupima vipimo vya kibingwa “hospitali ya Mkoa inatoa huduma za kibingwa saba (7), tunaye daktari bingwa wa magonjwa ya wanawake na uzazi (1), daktari bingwa wa magonjwa ya ndani (kisukari, pressure na moyo (1), daktari bingwa wa upasuaji (2), daktari bingwa wa magonjwa ya dharura (2) na daktari bingwa wa magonjwa ya sikio, pua na koo (1)”.
Dkt. Magali amemueleza Mhe. Mkuu wa Mkoa kwamba siku ya leo tumewaletea huduma ya utengamavu. Huduma hii inahusisha huduma za Physiotherapy (Fiziotherapia) pamoja na Occupational therapy (Tiba kwa vitendo). Ndugu wananchi mtakapofika kwenye banda letu mtaelezwa na mtaona namna vifaa tiba vya utengemavu vinavyofanya kazi. Dkt. Magali aliongezea kwa kusema mazoezi tiba yanatakiwa yawe yana utaalamu kwahivyo utapewa utaalamu wa namna ya kufanya mazoezi tiba bila kuumiza mwili wako. Wananchi wengine wanaweza kuwa na tatizo la paralysis (kupooza), na ukipata paralysis huwezi kufanya shughuli zako au watoto wengine wamepata utindio wa mbongo na ukipata utindio wa mbongo huwezi kufanya kazi zozote. Kwa hivyo kupitia wataalamu waliopo kwenye banda letu watakufundisha namna ya kuweza kujitegemea na kufanya shughuli zako kupitia mazoezi tiba.

“Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara imeanzisha huduma mpya ya ‘dharura’, ndugu wananchi napenda kuwatangazia popote pale utakapokuwa umepata ajali hospitali ya Mkoa wa Manyara ipo tayari kukufuata kwa kutumia ambulance yake, kwa hivyo tunaomba mtupigie simu sehemu yoyote ajali ilipotokea tutakuja kuwahudumia” Dkt. Magali alimalizia kwa kusema hayo.