DKT. KATHERINE MAGALI AMEPOKEA MASHUKA 79 KUTOKA VYAMA VYA USHIRIKA MKOA WA MANYARA
Posted on: June 21st, 2024Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara imepokea msaada wa mashuka 79 kutoka kwa Vyama vya ushirika mkoa wa Manyara siku ya leo tarehe 21/06/2024.
Akizungumza wakati wa kupokea msaada huo Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Katherine Magali amewashukuru Wadau kwa kutoa msaada huo ambao utaenda kusaidia utoaji huduma wa hospitali na kuiomba jamii iige mfano wa Wadau hawa.
Pia Bw. Yuda Sulle ambaye ni Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya vyama vya ushirika mkoa wa Manyara amemueleza Dkt. Katherine Magali kwamba, Vyama vya ushirika vimekuwa na utaratibu wa kutoa misaada mbalimbali katika jamii ikiwa ni kuunga mkono jitihada mbalimbali za serikali ikiwamo kuboresha Sekta ya Afya nchini.