Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

SIKU YA UKIMWI DUNIANI

image description

Thursday 25th, April 2024
@MANYARA

Maadhimisho ya siku ya UKIMWI DUNIANI.

Tume ya kuthibiti UKIMWI Tanzania (TUCAIDS) inaratibu maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani, ambayo hufanyika kila mwaka Disemba Mosi.

Madhumuni ya maadhimisho haya ni kutathmini hali na mwelekeo wa udhibiti UKIMWI Kitaifa na Kimataifa. Aidha, siku hii hutumika kuhamasisha na kuelimisha Jamii juu ya namna ya kujikinga na maambukizi mapya ya VVu, matumizi sahihi ya ARV kwa watu wanaoishi na VVu pamoja na kupinga unyanyapaa na ubaguzi.

Maadhimisho ya Kitaifa mwaka huu yatafanyikia Jijini mwanza ambapo Mgeni Rasmi atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa na hapa Manyara yatafanyika BABATI na SIMANJIRO MERERANI.

Kwa mujibu wa Shirika la UNAIDS, kauli mbiu ya maadhimisho haya ya mwaka huu ni "COMMUNITIES MAKE DIFEERENCE". Kauli mbiu hii imetafsiriwa kwa Kiswahili kuwa "Jamii ni Chachu ya Mabadiliko-Tuungane Kupunguza Maambukizi Mapya ya VVU"

Kauli mbiu hii inasisitiza ushirirki na ushirikishaji wa Jamii katika shughuli za udhibiti UKIMWI kuanzia kwenye upangaji mikakati, upatikanaji na utoaji wa huduma za VVU na UKIMWI.

JOIN HANDS TO FIGHT AIDS.