Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA AKILI DUNIANI

Wednesday 23rd, October 2024
@

Siku ya Afya ya Akili Duniani huadhimishwa na Jumuiya ya Kimataifa kila mwaka ifikapo tarehe 10 Oktoba kwa lengo la kuongeza uelewa wa matatizo ya afya ya akili duniani kote na kuhamasisha jitihada za kusaidia afya ya akili. Siku hii iliadhimishwa kwa mara ya kwanza tarehe 10 Oktoba 1992, kwa ushirikiano na Shirikisho la Afya ya Akili Duniani “World Federation of Mental Health” pamoja na kuungwa mkono na Shirika la Afya Duniani (WHO). Siku hii inatoa fursa kwa wale wote wanaohusika katika ngazi mbalimbali katika nyanja ya afya ya akili kuchunguza na kubadilishana uzoefu, mang’amuzi ya masuala muhimu na mapendekezo, ili kuchangia katika kufanya huduma kwa watu wenye matatizo ya akili kuwa halisi, inayopatikana, huduma inayojumuisha pamoja na kuleta ufanisi bora duniani kote.


Kauli mbiu "Ni Wakati wa Kuweka Kipaumbele cha Afya ya Akili Mahali pa Kazi."