Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

KLINIKI MKOBA YAEDA CHINI

Hospitali ya Mkoa inajukumu la kutoa huduma za Afya kwa wilaya zote za mkoa wa Manyara. Hospitali ya Mkoa kushirikiana na mradi wa Carbon Tanzania   imekuwa na utaratibu wa kutoa huduma ya kliniki mkoba kwa wanachi waishio katika bonde la yaeda chini. Kliniki ya mwisho ilifanyika mwezi wa mei 2019.

Hospitali imepanga kufanya zoezi hilo katika bonde la Yaeda chini Mbulu kuanzia tarehe 18/11/2019 hadi 22/11/2019. Huduma zitakazo tolewa ni upimajia wa maambulikizi ya virusi ya UKIMWI, Maambukizi ya ugonjwa kifua kikuu, Upimaji wa magonjwa ya shinikizo la damu sukari, magonjwa ya Macho na magonjwa yaliokuwa hayapewi kipaumbele.

Kwa tangazo hili, ukiona tafadhali mjulishe na mwingine.

- 14 November 2019