KAMBI YA MADAKTARI BINGWA MACHI 2024
Hospitali ya Rufaa Mkoa Manyara inapenda kuwatangazia wakazi wote wa Mkoa Manyara na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na huduma za Madaktari Bingwa kuanzia tarehe 25 hadi 29 Machi, 2024 zitakazofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara.
Hospitali inawatangazia wananchi wote wanaohitaji kupata huduma hizo wafike kwenye hospitali mapema kwa ajili ya uchunguzi wa awali na kupatiwa maelekezo ya namna ya kukutana na Madaktari Bingwa.