Zaidi ya 1800 wanufaika na kambi ya madaktari bingwa Manyara
Posted on: April 24th, 2026Zaidi ya wananchi 1800 wamenufaika kwa kufanyiwa uchunguzi na matibabu katika kambi maalum ya matibabu na upasuaji katika Hospitali ya Rufaa mkoa wa Manyara na kuhudumiwa na madaktari bingwa na wataalamu bobezi kutoka Marekani kuanzia april 19 hadi april 24,2026.
Hayo yameelezwa leo na Kaimu Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa mkoa wa Manyara Dokta Yesige Mutajwaa wakati akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake, amesema katika kipindi hicho cha Aprili 19 hadi Aprili 24 kumetolewa matibabu ya upasuaji maalum( plastic surgery ) kurekebisha makovu yaliyotokana na ajali au moto, matibabu ya mdomo sungura,upasuaji wa jumla, huduma za pua, sikio, koo, macho ,matibabu ya mifupa, matibabu ya magonjwa ya wanawake na uzazi pamoja na uchunguzi wa saratani.
Mutajwaa amesema katika kipindi hicho jumla ya wagonjwa 77 wamefanyiwa oparesheni katika maeneo mbalimbali ambapo amewashukuru wadau wote ambao wamepelekea kuendesha kambi hiyo.
Aidha, amewasisitiza wananchi kuendelea kufika katika vituo vya kutolea huduma za afya wanapohisi dalili za kuumwa ili wafanyiwe matibabu pamoja na ushauri kabla magonjwa hayajawa sugu.



