Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WANAWAKE WA MANYARA RRH WALETA FARAJA KWA WAGONJWA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Posted on: March 8th, 2026

Katika kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 08 Machi 2026, watumishi wanawake wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wameonesha moyo wa huruma na upendo kwa jamii kwa kufanya matendo ya kibinadamu kwa wagonjwa waliokuwa hospitalini hapo.

Katika tukio hilo, wanawake hao walitoa msaada wa maziwa ya watoto wachanga kwa akina mama waliolazwa hospitalini wakiwa na watoto wachanga, pamoja na kulipia gharama za matibabu (bili) kwa mwanamke mgonjwa aliyekuwa hana uwezo wa kulipa gharama hizo.

Sambamba na hilo, watumishi hao walipata wasaa wa kukutana na kusherehekea siku hiyo muhimu kwa pamoja, ambapo walijadiliana mambo mbalimbali ya kuimarisha mshikamano miongoni mwao na kuboresha utoaji wa huduma kwa jamii wanayoihudumia.

Maadhimisho ya mwaka huu yanaongozwa na kaulimbiu isemayo:

“Haki na Usawa kwa Wanawake na Wasichana: Msingi Jumuishi wa Kufikia Dira ya Maendeleo ya 2050.”