Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

TAKUKURU YATOA VIFAA TIBA KATIKA WODI YA WATOTO WACHANGA

Posted on: November 24th, 2025

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Tanzania (TAKUKURU) leo Novemba 24, 2025, imetoa vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara
kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya watoto wachanga walioko katika hali hatarishina wanaohitaji uangalizi maalumu. Vifaa hivyo, ambavyo ni phototherapy machine na infant radiant warmer,
vitasaidia kuongeza uwezo wa hospitali katika utoaji wa huduma muhimu za dharura kwa watoto wachanga na kuboresha zaidi mazingira ya matibabu kwa watoto wanaohitaji uangalizi wa karibu.