TABIA BWETE YATAJWA MOJA YA SABABU YA SHINIKIZO LA DAMU
Posted on: May 14th, 2026Hayo yameelezwa siku ya leo tarehe 14 Mei, 2026 na Dkt. Noel Nyelo wa Idara ya Magonjwa ya Ndani, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara katika cha kipindi cha elimu ya afya redioni @revivalfmtz .
Dkt. Nyelo ameeleza kwamba moja wapo ya sababu ya ongezeko la wagonjwa wa shinikizo la damu ni tabia bwete.
“kukaa sehemu moja muda mrefu, kutokufanya mazoezi husababisha mafuta mwilini kukaa sehemu moja na kupunguza mzunguko wake katika damu kisha kupelekea ugonjwa wa shinikizo la juu la damu” alieleza Dkt. Nyelo.
Aliongeza kwamba, sababu nyingine ni matumizi ya chumvi nyingi katika vyakula tunavyokula, unywaji wa pombe kupitiliza na uvutaji wa sigara huchangia shinikizo la juu la damu.
Dkt. Nyelo amesisitiza kwamba, upimaji wa afya mara kwa mara ni bora kwa sababu dalili za ugonjwa wa shinikizo la juu la damu hazipo wazi hadi pale hali inapokuwa mbaya.



