SIKUKUU YA WAUGUZI YAADHIMISHWA KWA MATENDO YA HURUMA NA KUCHANGIA DAMU
Posted on: May 12th, 2026Wauguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, wameadhimisha Sikukuu ya Wauguzi Duniani kwa kufanya matendo ya huruma kwa wagonjwa waliolazwa wodini pamoja na kushiriki zoezi la kuchangia damu.
Kila tarehe 12 Mei ya kila mwaka Wauguzi ulimwenguni kote huungana kushiriki Siku ya Wauguzi Duniani.
Kauli mbiu ya maadhimisho haya kwa mwaka huu 2026 inasema “Wauguzi wetu, Mustakabali wetu, Wauguzi waliowezeshwa huokoa maisha.”



