NAIBU WAZIRI WA AFYA AFANYA ZIARA NA KUTEMBELEA HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA
Posted on: November 26th, 2025Naibu Waziri wa Afya Mh. Dkt. Florence Samizi amefanya ziara mkoani Manyara leo tarehe 26 Novemba, 2025 na kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
Akiwa katika ziara yake ametembelea miradi mbali mbali iliyokamilika hapa hospitali na inayoendelea ikiwemo Ujenzi wa Jengo la Wagonjwa wa Dharura (EMD), Jengo la Wagonjwa wanao hitaji uangalizi wa karibu (ICU) pamoja na Jengo la Damu Salama, na kuagiza miradi hiyo ikamilike mapema ili kuongeza huduma bora kwa wananchi.
Aidha Mh. Dkt. Samizi aliambatana na Mh. Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Bi. Maryam Muhaji, Mbunge wa Babati Mjini Mh. Emmanuel Khambay, Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Andrew Method na Kaimu Mkurugenzi wa Tiba Wizara ya Afya Dkt. Mwinyi Amir.



