Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

MGANGA MKUU WA SERIKALI AFURAHISHWA NA HALI YA UTOAJI HUDUMA ZA AFYA HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA

Posted on: February 17th, 2026

Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe amefurahishwa na huduma za afya zinazotolewa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wakati wa ziara yake leo tarehe 17 Februari, 2026 alipofika hospitalini hapa.

Dkt. Magembe alitoa pongezi hizo wakati wa kikao na watumishi wa hospitali kikao kilichohudhuriwa na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Yesige Mutajwa, Katibu wa Afya Hospitali na Timu ya Uendeshaji wa Hospitali na Watumishi wa Hospitali. Dkt. Magembe alipongeza utoaji huduma wa hospitali baada ya kujiridhisha mwenyewe kwa kutembelea maeneo ya kutolea huduma na kuongea na wananchi mbalimbali wanaopatiwa huduma hospitalini hapa.

Pia Dkt. Magembe katika kikao hicho aliongelea swala la maadili ya utumishi UMMA ambapo alisema,

“kwenye maadili ya utumishi wa UMMA kila mtumishi anayo job description yake, sasa ni lazima tuzingatie kila mtu maadili ya kazi yake. Kila mtu alikula kiapo kwa kazi yake anayofanya, hivyo tuzingatie viapo vya kazi zetu ili tuweze kuwahudumia wananchi kwa namna ambayo inaendana na maadili ya wataalamu.”

Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara Dkt. Yesige Mutajwa alimweleza Dkt. Magembe kwamba, hospitali imekuwa ikitumia njia mbalimbali kukusanya maoni ya wateja ili ili kusaidia katika kuendelea kuboresha huduma zinazopatikana hapa hospitali.

Mifumo hii ni e-mrejesho, fomu za maoni, namba za simu za viongozi na kituo cha huduma kwa wateja, Dkt. Mutajwaa alieleza hayo.

Aidha, Dkt. Magembe katika ziara yake alitembelea jengo la Dharura (EMD) na jengo la Wagonjwa Mahututi (ICU) ambayo tayari yanaendelea kutoa huduma na kuridhishwa na ujenzi wa majengo hayo ambayo yako kwenye hatua za mwisho kukamilika.