Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

LESOTHO, UGANDA NA MALAWI WATEMBELEA MANYARA RRH KUJIFUNZA HUDUMA YA M-MAMA

Posted on: March 18th, 2026

Wageni kutoka Nchi za Lethoso, Uganda na Malawi wamefanya ziara leo tarehe 18 Machi, 2026, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kujifunza huduma ya mama na mtoto pamoja na mfumo wa M-Mama unavyotumika katika kumsafirisha mama mjamzito, mama aliyejifungua na mtoto mchanga.

Katika ziara hii walipata wasaa wa kutembelea Wodi ya wazazi, Kituo cha uratibu na usafirishaji wa dharura cha M-Mama na kufanya kikao kifupi hapo Hospitali.

Aidha, Wageni kutoka Nchi za Afrika waliambatana na Watumishi wa TAMISEMI, Wizara ya Afya, Wadau mbali mbali wakiwemo Vodacom Tz Foundation, Pathfinder, East Central & Southern Africa Health Community (ECSA) pamoja na Timu ya Afya Mkoa wa Manyara ikiongozwa na Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Andrew Method.