Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

ELIMU NA VIPIMO VYA PRESHA MNADANI GENDI

Posted on: May 17th, 2026

Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara leo tarehe 17 Mei 2026, ikiwa ni kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Shinikizo la Juu la Damu Duniani, imeweka kambi maalum katika mnada maarufu wa Gendi uliopo Babati kwa ajili ya kutoa huduma za vipimo vya shinikizo la damu, ushauri wa afya pamoja na elimu ya lishe bora kwa wananchi.

Huduma hizo zinalenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu madhara ya shinikizo la juu la damu na umuhimu wa kufanya uchunguzi wa afya mara kwa mara ili kubaini tatizo hilo mapema na kuchukua hatua stahiki za matibabu na kinga.

Wananchi waliojitokeza katika kambi hiyo wamepata fursa ya kupimwa bure, kupewa ushauri wa kitaalamu kuhusu mtindo bora wa maisha, lishe sahihi, pamoja na namna ya kujikinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza hususan shinikizo la juu la damu.

Huduma hii inaendelea kutolewa hadi jioni ili kuwapa wananchi wengi zaidi nafasi ya kufikiwa na huduma muhimu za afya pamoja na elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukiza.