Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WATUMISHI WA HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA KATIKA SIKU YA WAFANYAKAZI DUNIANI

Posted on: April 30th, 2025

Pichani ni Watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara katika matukio tofauti tofauti waliposhiriki Siku ya Wafanyakazi Duniani leo tarehe 30 Aprili 2025 katika Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Wilayani Babati mkoani Manyara. 

Mh. Queen Sendiga ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara alikuwa mgeni rasmi katika siku hii, akiambatana na Viongozi wengine wa mkoa, wilaya ya Babati na Taasisi mbalimbali za mkoa wa Manyara.

Siku ya Wafanyakazi kwa mwaka huu wa 2025 imebeba kauli mbiu “Uchaguzi mkuu 2025 utuletee viongozi wanaojali haki na maslahi ya wafanyakazi, sote tushiriki.”