Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WATUMISHI WA AFYA WAELIMISHWA MAMBO YA KUZINGATIA WAKATI WA UNYONYESHAJI WA MTOTO

Posted on: August 5th, 2024


Katika Maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji Duniani, Bi Josephine Mosha (Afisa Muuguzi Msaidizi) na Bw. Reginald Dinya (Afisa lishe) watumishi wa hapa hospitalini wameendelea kuelimisha umma umuhimu wa unyonyeshaji na lishe kwa mama aliyejifungua mtoto.


Ndani ya wiki hili walielimisha Watumishi wa hapa hospitalini, faida ya unyonyeshaji, aina ya vyakula na mambo ya kuepuka kwa mama anayenyonyesha mtoto.

Kila terehe 1 hadi 7 Agosti kila mwaka zaidi ya nchi 120 ikiwemo Tanzania huadhimisha wiki ya unyonyeshaji duniani. Kauli mbiu ya wiki ya unyonyeshaji mwaka huu, “Tatua Changamoto, Saidia Unyonyeshaji kwa Watoto.”