WANAWAKE MANYARA RRH WAFANYA MATENDO YA HURUMA KWA WAGONJWA NA WAFUNGWA
Posted on: March 8th, 2025
Wanawake kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara walisherehekea kilele cha Siku ya Wanawake Duniani hapo jana Machi 08, 2025 kwa kufanya matendo ya huruma na msaada kwa jamii, walikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wagonjwa, ikiwa ni pamoja na watoto, wamama wajawazito, pamoja na kuchangia fedha kwa ajili ya matibabu ya mgonjwa mmoja wa kiume.
Vilevile, wanawake hawa walitembelea Gereza la Babati kwa lengo la kuwaona wanawake wafungwa na kutoa mchango wa kiroho na mahitaji ya vitu mbali mbali kama Sabuni,Taulo za kike,mafuta,dawa za meno,miswaki, kanda mbili.
Baada ya kufanya matendo hayo ya huruma, wanawake hao walikusanyika pamoja kujadili masuala muhimu ya kuboresha umoja wao na kuendeleza mshikamano, Huu ulikuwa pia ni wakati mzuri wa kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani, ikiwa ni siku ya kutambua na kuthamini mchango wa wanawake katika Maeneo ya kazi na jamii kwa ujumla.
Kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani kwa mwaka 2025 ni " Wanawake na Wasichana Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji