WANAFUNZI WA KIDATO CHA 4 WAWAJULIA HALI WAGONJWA
Posted on: November 29th, 2024Wanafunzi waliohitimu Kidato cha nne mwaka 2024 katika Shule ya Sekondari Gallapo, Kata ya Gallapo, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, leo tarehe 29 Novemba 2024 wamefika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kuwajulia hali watoto waliolazwa na kukabidhi misaada ikiwa ni shukrani kwa kumaliza salama mitihani yao.
Katika hatua nyingine Wanafunzi hawa kwa kuongozwa na Mwalimu Erick Simba wa Shule hiyo wamepanda miti ya matunda katika eneo la hapa hospitali.
Mkuu wa Idara ya Watoto Dkt. Salha Nassor kwa niaba ya Uongozi ameshukuru kwa kitendo walichofanya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Gallapo na kuwa takia Heri kwenye maisha yao.