Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

WAGONJWA 365 WAMEPATIWA MATIBABU YA KIBINGWA WILAYANI SIMANJIRO

Posted on: November 25th, 2024

Katika kuhitimisha Kliniki Maalum ya Madaktari Bingwa wa Mkoa wa Manyara iliyoanza tarehe 18 Novemba 2024 na kuhitimishwa tarehe 22 Novemba 2024 katika Hospitali ya Wilaya ya Simanjiro jumla ya wagonjwa 356 walipatiwa matibabu.

Miongoni mwa Idara ambazo zilihudumia wagonjwa ni Idara ya Magonjwa ya Ndani wagonjwa (100), Idara ya Watoto (75), Idara ya Wanawake na Afya ya Uzazi (70), Idara ya Upasuaji (46) na Idara ya Macho wagonjwa (62). Huku kati ya idara hizo wagonjwa 7 wakifanyiwa upasuaji mkubwa.

Kliniki hizi ni katika muendelezo wa kuboresha afya za Watanzania ambapo maboresho makubwa yamefanyika kwenye Sekta ya Afya na Serikali ya awamu ya sita katika Uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Tarehe 19 Novemba 2024 Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mh. Queen Sendiga alizindua kwa mara ya kwanza, Kliniki Maalum ya Madaktari Bingwa wa Mkoa wa Manyara Wilayani Simanjiro na kueleza kwamba kliniki hizi zitafanyika kwenye Wilaya zote za Mkoa wa Manyara.