UPASUAJI, USTAWI WA JAMII WAWEKA KAMBI KATESH, HANANG’
Posted on: March 19th, 2024Katika muendelezo wa kuimarisha utoaji huduma za afya kwa wananchi, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kupitia Idara ya Upasuaji na Kitengo cha Ustawi wa Jamii wamepiga kambi Kijiji cha Kateshi Wilayani Hanang’ kwaajili ya kuhudumia wakaazi wa mahali hapo.
Kuanzia terehe 20 hadi 21 Machi mwaka huu zaidi ya wananchi 80 wamepimwa vipimo vya awali na waliogundulika na ugonjwa wameshauriwa na madaktari kufika hospitali kwaajili ya matibabu zaidi.
Aidha Wananchi wameelimishwa kuhusu maswala ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto pamoja na msaada wa kisaikolojia jamii.
Kliniki mbalimbali zimeendelea kufanyika na Wataalam wa Afya wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara ndani ya Mkoa kwa wananchi washio mbali na vituo vya afya na hospitali, lengo likiwa ni kuwafikia wananchi wasio na uwezo na kusogeza huduma karibu yao.