Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Msaada kwa wasiojiweza-Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara

Posted on: February 8th, 2020

Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Manyara, kupitia kwa Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt. Damas Kayera imewasilisha msaada kwa mgonjwa asiejiweza(jina limeifadhiwa) kwa kumpatia baiskeli ya walemavu ambayo ilifikishwa hapa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara tarehe 30, Januari, 2020 na Bw.Evance Simkoko kama mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa pamoja na uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara ukiongozwa na Dkt. Katherine T. Magali.

Bw. Evance Simkoko (wanne kutoka kushoto) na Dkt. Katherine T. Magali (wakwanza kutoka kulia) pamoja na wenginne walioudhuria katika kumjulia hali mgonjwa na kumfariji pia kwa kile walichoweza kukiwasilisha ili kumsadia mgonjwa kama inavyoonekana kwenye picha. (Picha na Celestine Marcel-Manyara).

Pamoja na hayo, waliweza kuongea machache na mgonjwa pia na ndugu zake wanaomsaidia wakati akiendelea na matibabu yake hapa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara. Mgonjwa (Jina lake limeifadhiwa) ametoa shukrani sana kwa uongozi mzima wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kupitia kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Manyara na Uongozi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara kwa kuweza kumsaidia kadili walivyoweza ili kumwezesha katika kukabiliana na shughuli zake hapo mbeleni.

Hospitali imetoa wito pia kwa watu walio na uwezo pamoja na taasisi mbali mbali kuweza kusaidia wale wenye uhitaji zaidi ili kupatiwa matibabu na kuwawezesha kurudisha matumaini yao katika utendaji wa shughuli zao hapo mbeleni.