KIBAYA YATEMBELEWA NA MADAKTARI BINGWA WA MKOA WA MANYARA
Posted on: February 18th, 2025
Pichani ni Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wakitoa huduma kwa wananchi katika Hospitali ya wilaya ya Kiteto (Kibaya) katika Kliniki Maalum ya Madaktari Bingwa wa Ndani ya Mkoa wa Manyara awamu ya pili, iliyoanza Jumatatu ya jana tarehe 17 Februari, 2025.
Kliniki hii ina jumuisha Madaktari Bingwa wa Magonjwa ya Ndani, Watoto, Pua, Sikio na Koo, Upasuaji, Macho, Wanawake na Afya ya Uzazi.