Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

KAMPUNI YA MATI SUPERBRANDS YAKABIDHI ZAWADI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MANYARA

Posted on: December 30th, 2022

KAMPUNI YA MATI SUPERBRANDS YAKABIDHI ZAWADI HOSPITALI YA RUFAA MKOA WA MANYARA

Katika kuadhimisha miaka mitano tangu kuanzishwa kwa @matisuperbrands , Uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo watembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara na kukabidhi zawadi mbali mabli pamoja na uchangiaji Damu.

Akiongea kwa niaba ya Uongozi wa Mati SuperBrand Bw. Goodluck Silayo ameiainisha kua katika maadhimisho ya miaka mitano ya kampiuni ya Mati SuperBrands wameonelea kuigusa sekta ya Afya kupitia Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kwa kukabidhi zawadi ikiwemo; jiko la gesi na umeme, maziwa ya Lactojeni, sabuni za maji na kitambaa kwaajili ya ushonaji wa sare za kina mama waliojifungua. 

Akipokea zawadi hizo kwa niaba ya uongozi wa Hospitali, Bi. Josephine Mosha (Muuguzi Mfawidhi) ameushukuru uongozi na timu nzima kutoka Mati SuperBrand kwa kuuona uhitaji katika sekta ya afya na kuamua kuigusa kwa namna hii. 

“Tunashukuru kwa jinsi mlivoamua kuadhimisha miaka mitano ya tangu kuanzishwa kwa kampuni yenu, tunawatakia kila la kheri. Hospitali haifungwi hivyo mkiguswa tena kwaajili ya wagonjwa mnakaribishwa sana, Mwenyezi Mungu awabariki” – Josephine Mosha (Muuguzi Mfawidhi)

#HudumaBoraniWajibuWetu