Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

KAIMU MGANGA MFAWIDHI AMEWAPONGEZA WAUGUZI WALIOHITIMU MAFUNZO YA DHARURA

Posted on: May 2nd, 2024

Wauguzi kutoka idara zilizopo Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wamehitimu mafunzo ya dharura (Emergence) yaliyoanza tarehe 29 Aprili 2024 na kuhitimishwa leo tarehe 2 Mei 2024.

Akizungumza wakati wa kuhitimisha mafunzo hayo Kaimu kwa niaba ya Uongozi wa Hospitali Bi. Vailine Oswald  amewapongeza wauguzi kushiriki katika mafunzo haya muhimu ambayo yana tija kubwa kwa Taasisi na pia yanawajengea uwezo wahudumu wa afya kukabiliana na huduma za dharura na jambo hili litakuwa endelevu, alisema Bi. Vailine Oswald.

Pia aliwapongeza Wauguzi waliohitimu kwa kuonesha ushirikiano mzuri na Wakufunzi ambao ni Bw. Wilson Lomnyack & Bi. Recipicia Katesigwa (kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili) na Bi. Ester Kindishe (kutoka KCMC) waliofika kwa ajili ya kutoa mafunzo hayo.

Naye Muuguzi Mfawidhi Bw. Msafiri Sehaba aliwasisitiza Wauguzi waliohitimu mafunzo haya kuendelea kutumia kile walichokipata katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kwamba wahitimu wa mafunzo haya ni mwanzo wa kupata walimu watakaoshiriki kutoa mafunzo mahala pengine.

Mafunzo haya yanasimamiwa na EMAT (Emergency Medicine Association of Tanzania) chini ya Wizara ya Afya na hufanyika nchi nzima kwenye Hospitali za Rufaa za Mikoa, dhumuni ni kuwajengea uwezo wahudumu wa afya, kuhudumia wagonjwa wa ajali, wenye changamoto ya kupumua na njia za kumuokoa mgonjwa.