Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

HOSPITALI YA MKOA WA MANYARA YASHIRIKI MICHEZO YA SHIMIWI

Posted on: October 7th, 2024

Watumishi kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara wameshiriki katika Timu ya Utumishi Sports Club, ambayo ipo chini Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika michezo ya SHIMIWI iliyofanyika mkoani Morogoro kuanzia Septemba hadi Oktoba 2024.

Timu hii ya Utumishi walishinda kwenye michezo ya mpira wa miguu, baiskeli na tufe ambapo mshindi wa kwanza baiskeli mwanaume alikabidhiwa kombe, mshindi wa pili mwanamke alikabidhiwa medali na mshindi wa tufe alikabidhiwa medali.

Michezo hii ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) ilijumuisha Mpira wa miguu, Mpira wa pete, Kamba, Draft, Riadha, Baiskeli, Mpira wa wavu, Karata, Dats na Bado ambapo ilifunguliwa tarehe 25/09/2024 na Mh. Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko mkoani Morogoro na kuhitimishwa tarehe 05/10/2024 na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mh. George Simbachawene (Mb).

Kauli mbiu ya mashindano ya SHIMIWI kwa mwaka huu ni “Michezo huongeza utendaji kazi, Shiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ujenzi wa Taifa Endelevu", ambapo haya ni mashindano ya 38.