ELIMU YA KINYWA NA MENO, NA FIZIOTHERAPI YATOLEWA KWA WATUMISHI WA NSSF MANYARA
Posted on: September 6th, 2022Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara kupitia idara za kinywa na meno, na fiziotherapi ilitoa elimu kwa watumishi wa NSSF Manyara. Zoezi hilo pia liliambatana na kueleza huduma mbalimbali zinazotolewa na idara hizo mbili (2)
Dkt. Stella Richard wa idara ya fiziotherapi alieleza mambo ambayo idara yake inafanya ikiwemo: kurekebisha mjongeo (movement maintenance), kurudisha mjongeo (movement restoration), fuctional ability improvement, na kutoa elimu ya kujikinga na magonjwa yasiyoambukizwa kama kisukari na pressure. Huduma zote hizi tunazitoa kwa watoto hadi wazee.
Haya ni baadhi ya magonjwa ambayo tumekuwa tukikutana nayo kwa wagonjwa wengi tunao wahudhumia yakiwemo: Maumivu ya mgongo wa chini ambayo yanatokana na kufanya kazi kwa muda mrefu,kukaa kwa muda mrefu na kusimama kwa muda mrefu. Maumivu mengine ni ya shingo, hutokea kwa watu ambao wanatumia kompyuta kwa muda mrefu. Magonjwa yote haya yanatibika na kupona. “Dkt. Stella Richard alieleza”
Pia tunavyo vifaa mbalimbali kwenye idara ya fiziotherapi kwaajili ya kutibu wagonjwa wanaofika hospitali. Traction machine ni moja ya kifaa tunachokitumia kutibu wagonjwa ambao disk zimekandamiza mishipa ya fahamu. Kifaa hiki hutumika kuvuta disk ili kusaidia kuondoa mkandamizo kwenye mishipa ya fahamu.
Gharama za huduma za fiziotherapi ni nafuu na unaweza kutumia bima za afya kwa matibabu.
Pia Dkt. Edward Magoma ambaye ni mkuu wa idara ya kinywa na meno alieleza huduma mbali mbali zinazotolewa na idara ikiwemo kuziba meno, matibabu ya mizizi ya meno, kutumbua jipu la jino na kung’oa meno. Pia idara inayo maabara kwaajili ya kutengeneza meno ya bandia.
Wagonjwa wengi tunaowahudumia wanafika wakiwa wamechelewa. Hivyo tunawasisitiza unapohisi dalili zozote za jino (kuuma,kutoboka na fizi kutoa damu) ni vyema kuwahi mapema hospitali ili kupunguza athari zaidi.
Mwisho, madaktari waliotoa elimu wasisitiza utunzaji bora wa meno kwa kusafisha kila baada ya kula na kwa upande wa fiziotherapi, msisitizo ulikuwa kufanya mazoezi mara kwa mara ya viungo na kuepuka kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu ili kupunguza matatizo mbali mbali yanayoweza kujitokeza kwenye viungo vya mwili.
Pia watumishi wa NSSF walipongeza hospitali ya rufaa ya mkoa wa Manyara kwa kuleta wataalamu wake kutoa elimu.