Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

UJIO WA MADAKTARI BINGWA MANYARA.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kupitia Hospitali ya Rufaa Mkoa Manyara inapenda kuwatangazia wakazi wote wa Mkoa Manyara na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na huduma za Madaktari Bingwa kuanzia tarehe 21 hadi 25 Juni, 2021 zitakazofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara.

Hospitali inawatangazia wananchi wote wanaohitaji kupata huduma hizo wafike kwenye Hospitali mapema kwa ajili ya uchunguzi wa awali na kupatiwa maelekezo ya namna ya kukutana na Madaktari Bingwa.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA NI PAMOJA NA MATIBABU YA:

  1. Magonjwa ya Pua, Sikio na Koo (ENT)
  2. Upasuaji

Kwa upande wa wanachama wa NHIF na bima nyingine watapata huduma kwa kutumia kadi zao na kwa wale wasio wanachama wa NHIF watachangia huduma hizo kwa utaratibu wa kawaida wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

UKISIKIA TANGAZO HILI TAFADHALI MTAARIFU NA MWENZAKO
- 10 June 2021