Barua Pepe | Facebook | Instagram | Twitter |

Kambi ya madaktari bingwa kuanzia tarehe 7 mpaka 11 Oktoba

Hospitali ya Rufaa Mkoa Manyara inapenda kuwatangazia wakazi wote wa Mkoa Manyara na maeneo ya jirani kuwa kutakuwa na huduma za Madaktari Bingwa kuanzia tarehe 7 hadi 11 Oktoba, 2019 zitakazofanyika katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Manyara.

Hospitali inawatangazia wananchi wote wanaohitaji kupata huduma hizo wafike kwenye Hospitali ya Rufaa Mkoa Manyara kwa ajili ya kupata huduma za Madaktari hao.

HUDUMA ZITAKAZOTOLEWA NI PAMOJA NA MATIBABU YA:

  1. Magonjwa ya Ndani (yaani Moyo, Kisukari, Presha )
  2. Magonjwa ya Watoto
  3. Magonjwa ya Wanawake na Uzazi
  4. Upasuaji
  5. Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo (ENT)
  6. Uchunguzi wa Saratani ya Kizazi na Uzazi wa Mpango

Kwa upande wa wanachama wa NHIF na bima nyingine watapata huduma kwa kutumia kadi zao na kwa wale wasio wanachama wa NHIF watachangia huduma hizo kwa utaratibu wa kawaida wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.

UKISIKIA TANGAZO HILI TAFADHALI MWARIFU NA MWENZAKO

- 04 October 2019